Utabiri wa Mvua za Msimu, Novemba mpaka Aprili 2018

Taarifa hii kama ilivyotelewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inatoa uchambuzi wa mifumo ya hali ya hewa na mwelekeo wa mvua za Msimu katika maeneo yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka katika kanda ya magharibi, kati, nyanda za juu kusini magharibi, maeneo ya kusini, ukanda wa Pwani ya kusini pamoja na maeneo ya kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Kutokana na mifumo ya hali ya hewa inayotarajiwa, mvua za wastani hadi juu ya wastani zinatarajiwa katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua kwa mwaka. Hata hivyo, vipindi vya mvua kubwa vinatarajiwa katika kipindi cha mwezi Januari 2018. Mvua hizi zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba na kuisha wiki ya nne ya mwezi Aprili 2018.

Mvua zinatarajiwa kuwa za wastani hadi juu ya wastani katika maeneo mengi ya mkoa wa Dodoma, Singida, Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Ruvuma, Lindi na Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro.

Katika maeneo ya mkoa wa Kigoma, Tabora, Rukwa, Katavi, Mbeya, Songwe, Njombe, Iringa, Lindi, Mtwara na kusini mwa mkoa wa Morogoro mvua zinatarajiwa kuanza wiki ya kwanza ya mwezi Novemba, 2017 na kusambaa katika mikoa ya Dodoma na Singida katika wiki ya kwanza ya mwezi Desemba, 2017.

Mtawanyiko hafifu wa mvua unatarajiwa katika maeneo ya Mikoa ya Lindi na Mtwara katika kipindi cha Januari hadi Februari, 2018 kipindi ambacho ukanda wa mvua unatarajiwa kuwa nje ya eneo la kusini mwa Tanzania. Mvua zinatarajiwa kuisha katika wiki ya mwisho ya mwezi Aprili, 2018 katika maeneo mengi yanayopata msimu mmoja wa mvua.

Athari za matukio ya vipindi vifupi vya mvua kubwa yanatarajiwa kusababisha mafuriko katika maeneo machache. Milipuko ya magonjwa inaweza kujitokeza kutokana na uhaba wa maji safi na salama na uwepo wa mfumo hafifu ya maji taka hususani katika mij.

Katika sekta ya Kilimo, hali ya unyevunyevu kwa ajili ya mazao na malisho ya mifugo na Wanyamapori inatarajiwa kuwa ya kuridhisha. Aidha, wazalishaji wa samaki wanashauriwa kutumia mbinu za kitaalamu katika ufugaji endelevu wa samaki. Wakulima na wafugaji.

Endelea kusoma taarifa zaidi hapa.

wanashauriwa kuvuna maji kipindi cha mvua kwa matumizi ya baadae.

Comments(2)

  1. Kazimoto kulwa simon says

    Congratulation for good information about our weather we need more specified weather information in geita region.

    • Coordinator says

      Thank you so much. We’ll link with TMA to get those specified weather information for your region geita.

Post a comment