UTABIRI WA MVUA ZA VULI (OKTOBA – DISEMBA, 2020) KWA WILAYA YA KASKAZINI “B”, UNGUJA

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa msimu wa mvua za Vuli katika kipindi cha Oktoba – Disemba, 2020 na athari zake kwa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi katika Wilaya ya Kaskazini “B”, Unguja.

Dondoo muhimu
• Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa katika Wilaya ya Kaskazini “B”, Unguja.
o Kwa kawaida wastani wa mvua katika miezi ya Oktoba – Disemba kwa Wilaya ya Kaskazini ‘B’ ni kati ya milimita 500 hadi 1000.
• Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2020.
• Hali ya upungufu wa mvua inatarajiwa mwezi Disemba, 2020.
• Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2021

Mvua za Msimu wa Vuli (2020) kwa Wilaya ya Kaskazini “B”
Zitaanza: Wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2020.
Zitaisha: Mwezi Januari, 2021.
Urefu wa Msimu wa Mvua: Kiujumla unatarajiwa kuwa mfupi.
Kiasi cha mvua zinazotarajiwa: Wastani hadi chini ya wastani
Kiwango cha juu cha mvua: Kinatarajiwa katika miezi ya Oktoba na Novemba, 2020.
Vipindi vya ukavu: Upo uwezekano wa kutokea vipindi vifupi vya ukavu kati ya wiki ya tatu na nne ya mwezi Disemba, 2020.
Mtawanyiko: Mvua zinatarajiwa kuwa na mtawanyiko wa kuridhisha katika maeneo mengi.

Angalizo:
­ Watumiaji wa taarifa hii wanashauriwa kufuatilia utabiri wa siku 10, saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

­ Wakulima, wafugaji na wavuvi wanashauriwa kupata ushauri zaidi kutoka kwa maafisa ugani kwa matumizi sahihi ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa.

Matokeo na ushauri kwa kilimo, mifugo na uvuvi
Matokeo
o Unyevunyevu ardhini unatarajiwa kuwa wa kuridhisha katika maeneo mengi hususan magharibi mwa wilaya Kaskazini B.
o Maji na malisho ya wastani kwa ajili ya mifugo yanatarajiwa, hata hivyo uwezekano wa upungufu kidogo kwa ukanda wa Mashariki unatarajiwa.
o Magonjwa ya mifugo, na wadudu waharibifu wa mazao yanaweza kujitokeza.
o Upatikanaji wa mazao ya baharini (samaki na mwani) unatarajiwa kuwa wa kawaida.
Ushauri
o Wakulima kutumia mbegu bora zinakomaa mapema na kustahmili magonjwa mfano viazi vitamu, kunde na mihogo kamavile, Kizimbani, Machui, kama na Mahonda.
o Wafugaji wanashauriwa kuhifadhi chakula kwa ajili ya mifugo ili kukabiliana na upungufu unaoweza kujitokeza.

Utabiri wa hali ya hewa nchini na tahadhari zinapatikana katika tovuti ya Mamlaka: www.meteo.go.tz

Mawasiliano yote yaelekezwekwa:
MkurugenziMkuu, Mamlakaya Hali ya Hewa Tanzania, Morogoro Rd, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3,
S.L.P. 3056, Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8.
Barua pepe: met@meteo.go.tz, Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)

You can also download the PDF form of this below
Pia unaweza kupakua utabiri huu hapo chini

Kaskazin B_ OND,2020_Final

Post a comment