UTABIRI WA MVUA ZA VULI (OKTOBA – DISEMBA, 2020) KWA WILAYA YA WETE, PEMBA

Taarifa hii inatoa mwelekeo wa mvua za Vuli katika kipindi cha Oktoba–Disemba, 2020 na athari zake kwa sekta za kilimo, mifugo na uvuvi katika Wilaya ya Wete, Pemba.

Dondoo muhimu
• Mvua za wastani hadi chini ya wastani zinatarajiwa Magharibi mwa Wilaya ya Wete.  Aidha, mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani hadi wastani mashariki mwa wilaya yaWete, Pemba.
o Kwa kawaida wastani wa mvua katika miezi ya Oktoba – Disemba kwa Wilaya yaWete ni kati ya milimita 500 hadi 1000.
• Mvua zinatarajiwa kuanza katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2020.
• Mtawanyiko mzuri wa mvua unatarajiwa katika kipindi chote cha msimu wa vuli,2020.
• Mvua zinatarajiwa kuisha mwezi Januari, 2021.

Mvua za Msimu wa Vuli (2020) kwa Wilaya ya Wete
Zitaanza: Katika wiki ya nne ya mwezi Oktoba, 2020
Zitaisha: Mwezi Januari, 2021.
Urefu wa Msimu wa Mvua: Unatarajiwa kuwa wa kawaida.
Kiasi cha mvua zinazotarajiwa: wastani hadi chini ya wastani Magharibi mwa Wilaya ya Wete.Aidha, mvua zinatarajiwa kuwa chini ya wastani hadi wastani Mashariki mwa Wilaya yaWete, Pemba.
Kiwango cha juu cha mvua: Kinatarajiwa katika mwezi Disemba, 2020.
Vipindi vya ukavu: Upo uwezekano mdogo wa kutokea vipindi vifupi vya ukavu mwanzoni mwa mwezi Oktoba, 2020.
Mtawanyiko: Mvua zinatarajiwa kuwa na mtawanyiko wa kuridhisha katika maeneo mengi.

Angalizo:
­ Watumiaji wa taarifa hii wanashauriwa kufuatilia utabiri wa siku 10, saa 24 pamoja na tahadhari kila zinapotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.

­ Wakulima, wafugaji na wavuvi wanashauriwa kupata ushauri zaidi kutoka kwa maafisa ugani kwa matumizi sahihi ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa.

Matokeo
o Hali ya unyevunyevu kiasi ardhini unaotarajiwa maeneo ya magharibi unaweza kutosheleza uzalishaji wa mazao ya mihogo, migomba na nanasi.
o Upungufu wa unyevunyevu wa udongo katika maeneo ya mashariki unaweza kuathiri uzalishaji wa mazao mfano mahindi na mtama.
o Magonjwa ya mifugo na wadudu waharibifu wa mazao hasa wakati wa msimu wa mvua yanaweza kujitokeza.
o Upungufu wa mvua hususan katika maeneo ya mashariki unaweza kuathiri upatikanaji wa malisho na maji kwa ajili ya mifugo.

Ushauri
o Wakulima wa maeneo ya miinuko wanashauriwa kutengeneza makinga maji na kuweka matandazo ili kuhifadhi unyevunyevu aridhini.
o Wakulima wa maeneo ya mashariki mwa Wete wanashauriwa kupanda mazao ya muda mfupi yakiwemo na jamii ya mikunde pia ni kipindi kizuri kwa kilimo cha mwani.
o Wafugaji wanashauriwa kutumia mvua hizo kwa ajili ya kupanda na kuhifadhi malisho.
o Wakulima wanashauriwa kutumia mvua hizi kupanda mazao ya kudumu, kama minazi na miti ya matunda.

Utabiri wa hali ya hewa nchini na tahadhari zinapatikana katika tovuti ya Mamlaka: www.meteo.go.tz

Mawasiliano yote yaelekezwekwa:
MkurugenziMkuu, Mamlakaya Hali ya Hewa Tanzania, Morogoro Rd, Ubungo Plaza, Ghorofa ya 3,
S.L.P. 3056, Dar es Salaam, Tanzania. Nukushi: +255 22 2460735, Simu: +255 22 2460706-8.
Barua pepe: met@meteo.go.tz, Tovuti: www.meteo.go.tz
(IMETHIBITISHWA – ISO 9001:2015, Huduma za Hali ya Hewa kwa Usafiri wa Anga)

You can also download the PDF form of this below
Pia unaweza kupakua utabiri huu hapo chini

Wete_ OND_2020_Mafuru

Post a comment